Mazingira FM

Majani yanayodhaniwa ni dawa za kulevya yakamatwa kwenye roli la mafuta Bunda

15 July 2024, 9:27 pm

Sehemu ya shehena ya magunia yaliyokamatwa yanayodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya, Picha na Edward Lucas

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Bunda kwa kushirikiana na mamlaka ya dawa za kulevya Kanda ya Ziwa wamekata magunia 205 yanayodhaniwa kuwa dawa za kulevya.

Na Edward Lucas

Shehena ya magunia 205 yenye majani makavu yanayodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya aina ya bangi yamekamatwa wilayani Bunda yakiwa yamepakiwa ndani ya tanki la roli la mafuta yakisafirishwa kutoka wilaya ya Tarime kwenda jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Naano, Picha na Edward Lucas

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Bunda ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya Dkt. Vicent Naano amesema roli hilo limekamatwa leo kufuatia ushirikiano wa mamlaka ya dawa za kulevya Kanda ya Ziwa kwa ushirikiano na vyombo vingine vya dola.

Sauti ya DC Dr Vicent Naano
Wakili wa serikali mkuu Christina Rweshabula, Picha na Edward Lucas

Kwa upande wake wakili wa serikali kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya nchini DCEA,  Christina Rweshabula amesema kwa sasa wanasubiri mkemia mkuu wa serikali kuthibitisha kama ni bangi au dawa zingine za kulevya.

Sauti ya wakili Christina Rweshabula