Wazazi watakiwa kuzingatia lishe kwa watoto
21 June 2024, 1:19 pm
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi kuzingatia lishe bora kwa watoto chini ya miaka mitano ili kuwa na watoto wenye afya bora
Na Catherine Msafiri
Wazazi na walezi wameaswa kuhakikisha wanazingatia lishe bora kwa watoto wao hasa wa mwaka 0 hadi miaka 5 Ili kuwakinga na utapiamlo na athari zitokanazo na tatizo hilo hayo yameelezwa na Albinus Manyama Chikwakala ambaye ni mwenyekiti wa wahudu wa afya ngazi ya jamii katika maadhimisho ya siku ya lishe ambayo hufanyika kwa mwaka mara mbili.
Akizungumza na Mazingira Fm Chikwakala amesema wao kama watoa huduma za afya ngazi ya jamii huwa wanayoa huduma nyumba Kwa nyumba Ili kuhakikisha wanawahimiza wazazi na walezi katika kuzingatia lishe bora kwa watoto wao na hata familia kwa ujumla.
Sambamba na zoezi la utoaji elimu pia kumefanyika zoezi la utoaji matone na dawa za minyoo kwa watoto chini ya miaka 5 Hadi miezi 6 ambapo Veronica Mathias muhudu wa afya ngazi ya jamii anawakumbusha wazazi kujitokeza kupata elimu na watoto wapewe chanjo kwa ni salama na zinawakinga watoto na maradhi mbalimbali.
Hata hivyo mwenyekiti wa mtaa wa Saranga Philipo Safari amesema kuwa zoezi hilo la utoaji elimu lishe kwa akina mama linatija na litakuwa endelevu ili kuhakikisha wanawaongoza wananchi wenye afya bora katika jamii.
Awali akifungua zoezi hilo mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Kabarimu Mhe Muhunda Manyonyoryo ameeleza mambo matatu ambayo wazazi wanapaswa kuyazingatia katika suala la malezi ya watoto hasa katika kuwapa lishe bora