Mrida; serikali inatushirikisha sisi wafugaji
10 May 2024, 6:33 pm
Kwa mwaka wa 2023 ha 2024 zaidi ya majosho 246 nchi nzima hii inaonesha serikali inawajali wafugaji.
Na Adelinus Banenwa
Mwenyekiti wa wafugaji taifa Ndugu Mrida Mshota amewataka maafisa mifugo kuwatembelea wafugaji na kuwapatia elimu badala ya kukamata mifugo yao.
Ndugu Mrida ameyasema hayo leo ndani ya kipindi cha Duru za Habari May 10, 2024 kinachorusha redio Mazingira Fm ambapo amesema jukumu la maafisa mifugo kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji ikiwa ni pamoja ana kutopitisha mifugo katikati ya barabara.
Katika hatua nyingine mrida amesema wao kama chama cha wafugaji wanaishukuru serikali kwa kuwa inawashirikisha kila hatua ya mipango ya maendeleo inayofanyika akitolea mfano ushiriki wao kwenye bajeti ya mifugo na uvuvi inayotarajiwa kusomwa bungeni May 14 2024.
Aidha mwenyekiti huyo amewataka wafugaji kuendelea kufuga vizuri lakini kuzingatia ufugaji wa kisasa wenye tija kama ni ng’ombe wa maziwa, nyama pia wafugaji wawe na maeneo ya marisho.