Mlida: Aainisha mipaka kuondoa migogoro wahifadhi na wafugaji
17 October 2023, 8:51 am
Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi shirika la NARCO Mhe Mlida Mshota ameziomba mamlaka kuainisha mipaka baina ya hifadhi na maeneo ya wafugaji ili kuepusha migogoro baina yao na wafugaji.
Na Adelinus Banenwa

Mhe Mlida amesema ili kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji au wahifadhi na wafugaji hakuna budi wafugaji kufuata sheria na kuheshimu mipaka.
Aidha Mlida ameeleza kuwa wafugaji wanatakiwa kuwa makini Kwa kuwa huko hifadhini wanyama wanamagonjwa mengi hivyo wakichanganyikana na mifugo yao inaweza kusababisha milipuko ya magonjwa.
Mlida ameiambia Mazingira Fm kuwa ana taarifa kuwa ng’ombe zaidi ya mia tatu (500) wameshikiliwa katika hifadhi ya taifa ya Serengeti upande wa Bunda baada ya kukamatwa hifadhini.
Katika hatua nyingine kupitia Mwenyekiti wa kamati ya malisho Tanzania George Saimon Kifuko amesema serikali hasa ngazi za wilaya na mikoa kuwathamini wakulima na kuwatengea maeneo ya Malisho ili kuondoa migogoro baina yao na wakulima