Katibu tawala Bunda ateta na wakuu wa shule Bunda mji
31 August 2023, 11:13 am
Kiongozi bora halalamiki bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya watu walio chini yake. kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.
Na Thomas Masalu
Imeelezwa kuwa kipimo cha uongozi ni jinsi gani kiongozi anaweza kuleta ushawishi kwa watu na kufikia maendeleo yaliyotarajiwa.
Kiongozi bora halalamiki bali anatafuta ufumbuzi wa matatizo ya watu walio chini yake.
Hayo yamesemwa leo na katibu tawala wilaya ya Bunda, mheshimiwa Salum Mtelela wakati akizungumza katika uwasilishaji wa mada ya uongozi katika kikao cha wakuu wa shule Bunda Mji, ukumbi wa landmasters.
Kwa mujibu wa tume ya haki za binadamu na utawala bora inaeleza kuwa utawala bora ni matumizi ya mamlaka ambayo yanakuwa na uwazi, uwajibikaji, ushirikishaji wa watu, ufanisi, tija, uadilifu usawa na unafuata utawala wa sheria.
Ili kutekeleza dhana ya utawala bora ni vyema ukazingatia misingi hii ambayo ni matumizi sahihi ya dola, matumizi mazuri ya rasilimali kwa faida ya wananchi, matumizi mazuri ya madaraka yao, kujua na kutambua madaraka waliyonayo na matumizi yake, madaraka yanatumika kulingana na mipaka iliyowekwa na katiba na sheria.