Mazingira FM

Mkurugenzi Bunda DC amaliza mgogoro eneo la ujenzi wa sekondari Nyaburundu

28 May 2023, 7:42 pm

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Mhe Changwa Mkwazu amemaliza sintofahamu ya eneo la ujenzi wa shule ya sekondari katika Kijiji Cha Nyaburundu Kata ya Ketare Halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika shule ya msingi Nyaburundu 27 Mei, 2023 Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bunda amesema kwa maelekezo ya mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano amefika kuwasikiliza wananchi wa Nyaburundu juu ya changamoto ya sehemu ya kujenga shule ya sekondari

Mkwazu amewaeleza wananchi kwamba anafahamu changamoto wanazozipata wanafunzi katika eneo hilo ila kwa maelekezo ya ngazi za juu hawatakiwi kuanzisha shule mpya jambo litakalosababisha uhitaji mkubwa wa Fedha za kuendesha mradi huo angali mapata ya halmashauri hiyo kwa mwaka ni shilingi 1.2 bilioni .

Changwa Mkwazu DED Bunda DC

Aidha Mkurugenzi amesema kupitia maelekezo ya mkuu wa Wilaya ya Bunda amepima eneo hilo na amewaruhusu wananchi kujenga shule ya sekondari katika eneo hilo ila kwa kufuata masharti waliyokubaliana

Naye mwenyekiti wa Kijiji Cha Nyaburundu Hamis Said Madoro amesema anashukuru uamuzi wa Mkurugenzi kwa kuwa changamoto hiyo ilikuwa tayari imeleta shida

HAMISI SAID MADORO mwenyekiti nyaburundu

Nao wananchi wameishukuru serikali kupitia kwa Mkurugenzi kusikiliza kilio Chao na wamesema waliokubaliana watayafanya Wala hawatamuangusha

Mussa Stephano Mwananchi wa nyaburundu
CHRISTINA DAUDI, MKAZI WA NYABURUNDU