DAS Bunda, maafisa kilimo toeni elimu kwa wakulima matumizi sahihi ya viuadudu kwenye zao la pamba
13 March 2023, 8:43 am
Katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Halfani Mtelela amewataka maafisa kilimo ngazi ya halmashauri na kata kuwaelimisha wakulima namna bora ya kutumia pembejeo za kilimo zinazoletwa na serikali hasa katika zao la pamba.
Hayo ameyasema wakati akipokea viuatilifu vya zao la pamba takribani ekapac elfu 50 vyenye thamani ya shilingi milioni 225 kutoka bodi ya pamba Tanzania kwa lengo la kuongeza uzalishaji kwenye zao la pamba wilayani Bunda.
Mhe Mtelela amewaelekeza maafisa ugani (kilimo) kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuadudu vilivyoletwa na bodi ambapo amesema imekuwepo changamoto kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya sumu hizo jambo linalopelekea usugu kwa baadhi ya wadudu kama vile chawajani.
Naye mkaguzi wa zao la pamba wilaya ya Bunda kutoka boda ya ya pamba Tanzania Hemed kabea amesema bodi ya pamba imekabidhi viuadudu hivyo kwa serikali kwa kuwa ofisi ya mkuu wa wilaya ndiyo yenye dhamana ya ufuatiliaji na ulinzi wa mali hiyo kuhakikisha haihujumiwi.