Mazingira FM

Mwenge wa uhuru wazindua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2.Bunda

7 July 2022, 9:17 pm

Mwenge wa Uhuru uwapo katika Halmashauri ya Mji wa Bunda tarehe 05.07.2022 umetembelea na kukagua Miradi mbalimbali, Umeweka jiwe la Msingi na kuzindua Miradi nane yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2.2.

Miradi iliyozinduliwa ni madarasa matatu na Ofisi moja yaliyojengwa kwa fedha za Uviko.

Madarasa mawili na Ofisi moja yaliyojengwa kwa Nguvu za Wananchi na kukamilishwa na fedha za Tozo.

Miradi iliyowekwa jiwe na Msingi ni mradi wa Zahanati ya Kisangwa, mradi wa Kiwanda Cha Laleo Company Ltd Cha Kukoboa na kusaga Nafaka na kutengeneza vyakula vya mifugo, Mradi wa Maji Bitaraguru, Mradi wa Shule ya Sekondari Nyamakokoto na Daraja la Barabara ya Machinjio.

Mwenge wa Uhuru ulitembelea pia mradi wa Kikundi Cha Vijana Cha African Top shine Kabarimu kinachojihusisha na utengenezaji wa mafuta ya nywele, sabuni ya unga na shampoo lakini pia ni Moja ya vikundi vilivyonufaika na mkopo wa Halmashauri wa asilimia kumi.

Mwenge wa Uhuru ulikesha katika Viwanja vya Stendi Mpya ambako Wananchi walijumuika kuushangilia hadi majira ya asubuhi.

Mwenge wa Uhuru Hoyeeee….

#kaziiendeleee
#sensa2022jiandaekuhesabiwa