Grumet Fund watoa somo utunzaji wa mazingira
6 June 2024, 8:00 am
Mazingira yakitunzwa vizuri jamii itaepukana na majanga mbalimbali kama vile vimbunga, mafuriko, ukame wa muda mrefu magojwa ya kansa miongoni mwa majanga mengine.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa wananchi kutunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hayo yamesemwa na bi Stellah Shabani Masakilija Kaimu afisa maliasili uhifadhi wa mazingira kutoka halmashauri ya Bunda mji kwenye kwenye studi za radio mazingira fm kupitia kipindi cha kapu letu siku ya kilele cha siku ya mazingira tarehe 5 June 2024.
Masakilija amesema mazingira yakitunzwa vizuri jamii itaepukana na majanga mbalimbali kama vile vimbunga, mafuriko, ukame wa muda mrefu magojwa ya kansa miongoni mwa majanga mengine.
Kwa upande wake Hasani Mtunzi ambaye ni afisa mahusiano kutoka shirika la Grumet Fund amesema wao kama taasisi wamewekeza kwa jamii katika utoaji wa elimu namna bora ya utunzaji wa mazingira kwa kushirikiana na serikali .
Amesema katika elimu wanayoitoa wamejikita katika makundi makuu matatu ambayo ni wazee, akina mama pamoja na watoto ambao ni wanafunzi lengo ni kila mmoja kwa nafasi yake ashiriki katika utunzaji wa mazingira hasa kulinda vyanzo vya maji.
Ikumbukwe kwamba siku ya mazingira duniani huadhimishwa kila tarehe 5 june kila mwaka ambapo mwaka huu kauli mbiu inasema Ulishwaji wa ardhi pambana na hali ya jagwa na ustahimilivu wa ukame.