Mazingira FM

Bunda: Wabunge wa Bunda walalamikiwa kuikwepa jumuiya ya wazazi CCM wilaya

1 January 2023, 5:42 pm

 

Leonard Magwayega, Mwenyekiti Jumuiya ya wazazi CCM Bunda

Jumuhiya  ya wazazi CCM Bunda imewatupia lawama wabunge wa wilaya ya Bunda kwa kushindwa kuwaunga mkono katika vikao vyao

Hayo yamebainishwa leo na Mwenyekiti wa Jumuhiya hiyo ndugu Leonard Magwayega wakati wa kikao cha baraza la umoja huo kilichofanyika kwa lengo la kuwachagua wajumbe wa baraza la utekelezaji miongoni mwa mambo mengine

Magwayega amewataka wajumbe wa baraza la jumuhiya hiyo kubuni miradi ya maendeleo itakayoisimamia jumuhiya hiyo ili waache kuwa ombaomba

KATIBU JUMUIYA YA WAZIZI CCM BUNDA

amedai licha ya kuwashirikisha wabunge juu ya uwepo wa baraza hilo lakini mara kadhaa hawaoneshi ushirikiano na wakati mwingine hawapokei simu

” mi nashangaa sana huenda hawa wabunge wametuchoka lakinimbona jumuiya ya akinamama UWT wanawachangia na hata jumuiya ya vijana UVCCM wanachanga iweje kwetu jumuiya ya wazazi hawataki kutuunga mkono lazima tubuni miradi yetu ili tuache kuwa ombaomba” alisema mwenyekiti Magwayega

“Mimi nataka katika kipindi changu tuweze kusimama kwa miguu yetu wenyewe tuache utegemezi wa mifuko ya watu maana ninachojua jumuiya hii ina wataalamu wote ikiwa ni watu wa kilimo na mifugo, madaktari, walimu, wanasheria iweje tushindwe kusimama wenyewe sitakubali” aliongeza Magwayega

katika baraza hilo la kwanza la jumuiya ya wazazi kukaa baada ya uchanguzi ndani ya chama cha mapinduzi CCM kukamilika waliadhimia kuanzisha miradi kadhaa ikiwemo kuanzisha shule ya Awali (chekechea)