Mazingira FM

Chuo cha kisangwa tayari kwenye mfumo wa kupikia nishati mbadala.

21 April 2023, 7:31 am

Chuo cha maendeleo ya wananchi kisangwa FDC wameiomba serikali kuzungumza na watoa huduma wa nishati mbadala za kupikia ili waweze kumudu gharama za uendeshaji katika ununuzi wa nishati hizo.

Akizungumza na Mazingira Fm ofisini kwake leo 19 April 2023 mratibu wa mafunzo wa chuo hicho Frances Kusekwa iliyofika kujua wanafanyiaje kazi maelekezo yaliyotolewa na wizara ya ofisi ya makamu wa Rais  Muungano na Mazingira  juu wa taasisi zote za umma na za binafsi kutumia nishati mbadala kwenye kupika ifikapo 31 January 2024.

Mratibu huyo amebainisha kuwa chuo cha kisangwa tayari kinao mfumo wa nishati mbadala kwa ajili ya kupikia ambapo mfumo huo ulianza kutumika tangu mwezi Decemba 2022.

Frances ameeleza kuwa mfumo huo umesaidia kupunguza changamoto ya kukata miti na uharibifu wa mazingira ambapo amesema kwa mwezi walikuwa wakitumia hadi kiubiki mita 10 hadi 20 za kuni kupikia sawa na kuni za shilingi milioni moja kwa mwezi.

FRANCES KUSEKWA

Aidha amefafanua kuwa pamoja na uzuri wa nishati hiyo mbadala tatizo kubwa ni gharama za uendeshaji kwa kuwa mtungi wa gesi ulioko shuleni hapo unauwezo wa kutumika kwa miezi mitatu ambapo kuujaza unatakiwa shilingi milioni tatu laki moja na arobaini na mbili elfu (3,142,000).

FRANCES KUSEKWA

Kwa upande wake welema amina maboga mpishi katika chuo cha kisangwa amesema matumizi ya nishati mbadala kwa kupikia yamewasaidia sana hasa kuwahi kuivisha chakula lakini pia kuwapunguzia adha ya moshi ambao kupitia kuni ulikuwa unawaathiri wao kama wapishi.

WELIMA MABOGA