Mazingira FM

MENEJA TARURA BUNDA; Mifugo kupita barabarani kunaharibu barabara, adhabu ni elfu tano (5,000) kila mfugo au kifungo kisichozidi mwaka mmoja.

17 April 2023, 9:01 am

Upitishaji wa mifugo barabarani (kuswagwa) imetejwa kama chanzo cha uharibifu wa barabara zinazojengwa na wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA wilayani Bunda.

Akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara katika kata za mihingo na nyasura meneja wa TARURA wilayani Bunda Muhandisi Baraka Mkuya amesema tatizio la wafugaji kupitisha mifugo kwenye barabara ni changamoto kubwa sana licha kuwa ni kinyume cha sheria.

Baraka amesema sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2007 kanuni ya 6 inaelezezea kosa na adhabu ambapo kifungu cha 58 cha kanuni hiyo kimetoa adhabu kwa mtu atakayepitisha mifugo barabarani kuwa ni faini ya shilingi elfu tano kila mfugo au kifungo kisichozidi mwaka mmoja.

ENG BARAKA MKUYA

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dr Vicent Anney Naano amesema ni kweli upitishaji wa mifugo kwenye barabara kunaleta uharibifu mkubwa hivyo amewaelekeza TANROAD na mamlaka za serikali za wilaya kuelekeza wafugaji kutumia maeneo ya hifadhi ya barabara kupitisha mifugo yao badala ya kupitisha barabarani ambapo ameongeza kuwa wananchi wengi hawajui kwamba ni kosa kufanya hivyo.

DR, VICENT NAANO

Awali diwani wa kata ya Nyasura Magigi Samweli Kiboko amesema wao kama madiwani ili kulinda barabara watamuelekeza mkurugenzi kukaza sheria kwa kuwa kupitisha mifugo barabarani kunasababisha zisidumu.

MAGIGI SAMWELI KIBOKO