Mazingira FM

DC Bunda ; amuweka ndani mganga mkuu wa halmashauri kwa upotevu wa vifaa tiba vya hospitali.

14 April 2023, 7:55 pm

DR VICENT NAANO DC BUNDA

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Anney Naano memuondoa mganga mfawidhi wa hospital ya halmashauri ya wilaya ya Bunda na kumuweka ndandi mganga mkuu wa halmashauri kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa vifaa  tiba vya hospitali hiyo

Akizungumza na wakazi wa kata Nyamuswa halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo wananchi walikusanyika baada ya kupata taarifa za upotevu wa vifaa hivyo huku wakidai vingewasaidia kupata matibabu karibu na kuepusha gharama za kwenda mbali.

WAKAZI WA NYAMUSWA

Kwa upande wakediwani wa kata hiyo Mhe Ibrahimu Mganga Igai amesema ni jambo la kusikitisha kuona vifaa vya hospitali vinapotea ndani ya vyumba wakati mirango yote iko sawa na haijavunjwa huku akiwatupia lawama watumishi kuwa wanahusika na upotevu huo

IBRAHIMU MGANGA IGAI DIWANI NYANUSWA

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Anney Naano amewataka wananchi na wakazi wa Nyamuswa kuwa watulivu maana tayari ameanza kuchukua hatua kwa kumuweka ndani mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Bunda DMO huku akiwaondoa watumishi katika hospitali hiyo akiwemo Mganga mfawidhi.

Aidha ametupa lawama kwa wale wote wanaohusika na ubadhilifu wa miradi ya maendele ahuku akisema kinachofanyika ndani ya halmashauri  ni ushirikiano kati ya wenyeji na watumishi

’’ juzi nilikamata gari limebeba nondo za kujenga jingo la utawala ya wilaya kule kibara hilo gari ni la mwenyeji wa bunda ameshirikiana na watumishi kutorosha nondo pia wizi wa million miamoja kumi na saba  ( 117, 000,000) miradi yote ya bunda ni wizi tu sitakubari tutachukua hatu”

DR VICENT NAANO DC BUNDA