Mazingira FM

Mbunge Mabotto ; ameitaka serikali isione haya kuwalipa wakazi wa nyatwali stahiki zao kwa kuwa siyo wavamizi.

26 February 2023, 11:20 am

MBUNGE WA JIMBO la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Mabotto ameitaka serikali isione haya kuwalipa wakazi wa nyatwali stahiki zao kwa kuwa siyo wavamizi.

Akizungumza katika kikao cha wananchi kilichoitishwa na mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Naano ambapo lengo ni kuangalia changamoto zinazojitokeza katika kipindi cha Uthamini.

Wakizungunza katika kikao hicho wananchi wamelalamikia wataalamu wanofanya tathmini kupunguza ukubwa wa maeneo yao amabapo wameeleza kuwa unaweza ukawa na ekari 10 lakini wathamini wakasema unazo ekari sita au saba.

Aidha wamesema changamoto nyingine ni malipo kidogo ambapo ekari moja inalipwa kwa shilingi milioni mbili 2,000,000 ambapo ukifanya mahesabu mita mija ya mraba inauzwa kwa shilingi mia nne na tisini na saba 497 wakati eneo hilo lipo Halmashauri ya mji wa Bunda ambapo kupitia baraza la madiwa walipitisha mita moja ya mraba ndani ya halmashauri hiyo iuzwe kwa shilingi elfu mbili na mia mbili 2,200.

Eneo la Mjapani, eneo la malisho maarufu kama Magwata, eneo la Mwabudoto maarufu kama Masanga na suala la kikokotoo cha uchakavu wa nyumba ni miongoni mwa hoja zingine walizosema ni changamoto katika uthamini.

Kwa upande wake mbunge wa Bunda mjini Mhe Robert Mabotto amesema serikali isione  haya kulipa watu fedha zinazostahili kwa kuwa nyatwali ni mgodi usiyoisha na kwa kuwa wao siyo wavamizi

Mhe Mabotto pia amesisitiza serikali kuangalia kwa amakini kwa kuwa katika zoezi hili yameanza kujitokeza masuala ya Rushwa ambapo baadhi ya wathamini wanatuhumiwa kuwaomba rushwa baadhi ya wannchi ili wawafanyie tathmini vizuri ikiwemo suala la kikokotoo cha uchakavu wa jengo.

Naye mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano amesema kwa yeyote ambaye uthamini hajaridhika nao timu hiyo itarudi kufanya tathmini upya, kwa kuwa yeye kama mkuu wa wilaya hawezi kukubali mwananchi ana ekari 10 kumi kisha akaandikiwa 5 tano lakini pia amewataka wakazi wa nyatwali kuendelea kushirikiana na serikali katika kumaliza jambo hili kwa amani maana kila mwananchi atapewa haki yake inayostahili.

Mkuu wa wilaya akiwa ameongozana na kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Bunda amesema jambo la Rushwa halikubaliki katika zoezi hili na kwa yeyote atakayehusika hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

 Amesema mjadala bado unaendelea kuhusu suala la Nyatwali ambapo amesema milango ya mazungumzo na majadiliano bado ipo kuhakikisha wakazi hao wanahama mwa furaha bila changamoto yoyote.