Mazingira FM

Aliyeshikwa na mamba Nyatwali apatikana akiwa amepoteza maisha.

20 February 2023, 2:52 pm

Wakaazi wa Nyatwali wakimsikiliza katibu tawala wilaya ya Bunda baada ya kupatika kwa mwili wa Maleba aliyeshikwa na mamba

Zoezi la utafutaji wa nduguĀ  Mayila Maleba mwenye umri wa miaka (37) aliyekamatwa na mamba wakati akiendelea na shughuli za uvuvi wa samaki kandokando ya ziwa Victoria eneo la Tamau,wamefanikiwa kumpata akiwa amepoteza maisha.

Jitihada za wakazi wa Nyatwali kumtafuta Maleba zazaa matunda baada ya kuupata mwili wake

Mwili umekabidhiwa kwa ndugu ili taratibu za mazishi ziendelee.

Mwanamme huyo ambaye alikamatwa siku ya jana jumapili tarehe 19 Feb 2023 majira ya saa 3:00 asubuhi wakati akiwa anavua samaki katika mpaka wa eneo la mtaa wa Tamau na Nyatwali akiwa kwenye mtumbwi mdogo maarufu kama denge ambapo juhudi za wananchi waliokusanyika kwa ajili ya kumtafuta wamefanikiwa kuupata mwili wake.