Mazingira FM

Mbunge Mabotto; Atoa zaidi ya milion 6 kuwasaidia wanafunzi wasiyojiweza jimbo la Bunda Mjini

10 January 2023, 5:10 pm

 

Zaidi ya shilingi million 4 laki 1 na 35 elfu zimetolewa na mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Mhe Robert Chacha Mabotto kwa wanafunzi 64 kwa ajili ya mahitaji yao ya shule.

Akizungumza kwa niaba ya mbunge wakati wa kukabidhi msaada huo katibu wa mbunge Peluth Mwita Kilanga amesema ni kawaida ya mbunge kusaidia wananchi wanyonge ndani ya jimbo lake nahii leo ametoa takribani shilingi million 4.1 kwa wanafunzi 64 ili waweze kukamilisha mahitaji yao ya shule.

 

Aidha Peluth ameongeza kuwa mnamo tarehe 6 mwezi huu  mbunge pia alitoa shilingi million  2.7 kwa watu 26 kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi.

Peluth amewataka wazazi na walezi waliopokea fedha kwa ajili ya kununua mahitaji hayo ya watoto kufanya hivyo ili wanafunzi waweze kufika shuleni kwa wakati.

 

Kwa upande wao wanafunzi na wazazi waliopokea msaada huo wamemshukuru mbunge kwa kuonesha moyo wa huruma kwao kwa kuwa hawakujua ni namna gani watoto wao wataenda shuleni wakati mahitaji hawana kama vile madaftari, mabegi ya shule, viatu miongoni mwa mahitaji mengine.