Mazingira FM

Bunda: CCM Nyasura yapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani 2022

17 December 2022, 2:38 pm

Halmashauri kuu ya ccm kata ya nyasura ikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho Marko Mabula Budosera imepokea taarifa aya utekerezaji wa ilani ya chama hicho kwa mwaka 2022

Akisoma taarifa hiyo mbele ya wajumbe wa halmashauri kuu hiyo afisa mtendaji wa kata ya Nyasura Elisha Henry amesema shughuli mbalimbali za maendeleo zimefanyika kwa mwaka 2022 katika Nyanja za elimu, miundombinu ya barabara,maji, ardhi umeme miongoni mwa shughuli nyingine.

 

Kwa upande wao wajumbe wa halmnashauri kuu hiyo wamehoji juu ya wanafunzi wa secondary ya Dr. Nchimbi kukutwa wanabeba mchanga na maji katika ujenzi wa madarasa ya sekondari hiyo angali serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa madarasa hayo.

Akijibu baadhi ya hoja diwani wa kata hiyo Mhe Magigi Samweli Kiboko amesema ni kweli wanafunzi walihusika katika kusogeza baadhi ya viashiria vya ujenzi wa madarasa kwa kuwa wananchi wamekuwa wagumu kujitokeza kusaidia kazi hiyo ambapo ukilinganisha bajeti ya ujenzi na gharama halisi ni tofauti hivyo shughuli zingine zinaitaji nguvu ya wananchi.

Mhe Kiboko amewaomba wanachama wote wa CCM na wananchi wa kata ya Nyasura kuendelea kushirikiana na viongozi ili kuleta maendeleo katika kata hiyo