Baraka FM
Baraka FM
20 August 2026, 22:27

kutokana na ongezeko kubwa la watumiaji wa mitandao ya kijamii vijana wanaendelea kuhimizwa kuacha kutumia mitandao hiyo kinyume na maadili ya jamii.
Na Ezra Mwilwa
Mahakama ya wwanzo Mbeya mjini imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja (miezi 12) jela Ramadhan Rudabuka (19) DJ na mkazi wa Patamela wilayani Chunya kwa kosa la kusambaza maudhui yasiyofaa katika mtandao wa TikTok.

Hukumu hiyo imetolewa mbele ya hakimu wa Mahakama ya mwanzo Mbeya mjini Mhe Ayubu Shirima.
Inaelezwa kuwa mshitakiwa alijirekodi na kusambaza maudhui yasiyofaa kwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya viongozi wa Serikali kwa lengo la kupata wafuasi wengi katika akaunti yake ya TikTok.
Mheshimiwa hakimu alitoa adhabu hiyo kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na watu wengine wenye tabia kama hiyo katika matumizi ya mitandao ya kijamii.