Baraka FM

Tumieni fursa vyuoni kuwa viongozi wa badae

23 November 2023, 17:44

Baadhi ya washiriki wa semina ya vijana chuo kikuu Teofilo Kisanji “TEKU“Mbeya (picha na Ezra Mwilwa)

Na Ezra Mwilwa

Vijana Waliopo vyuoni wameshauriwa kujianda na masuala ya uongozi katika nyanja Mbalimbali za kijamii.

Wito huo umetolewa na Mch.Agines Njeyo katika semina iliyoandaliwa na Wanafunzi wa Makanisa ya CCT Chuo kikuu Teofilo Kisanja ambapo amesema katika nyakati hizi vijana wanatakiwakujiandaa kuwa Viongozi bora katika sehemu tofauti za kijamii.

Mch.Njeyo amesema viongozi wa kanisa wanaandaa semina mbalimbali ili kuwaelimisha vijana juu ya masuala ya uongozi pamoja na uchumi wao binafsi.

Mch.Agines Njeyo
Sauti ya Mch.Agines Njeyo

Kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wanafunzi CCT Abel Mlibo amesema wamefanya semina ya kijana na uongozi kutokana na uhitaji wa viongozi kila idara.

Sauti ya mwenyekiti wa umoja wanafunzi CCT Abel Mlibo

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wamesema wamejifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na kila kijana kujiaanda kuwa kiongozi na kuwa kiongozi bora katika sehemu atakayokuwepo.

Sauti za Baadhi ya washiriki wa semina