Baraka FM

Wananchi watakiwa kuendelea kuitunza amani

8 April 2024, 18:37

Baadhi ya wakuu wa wilaya mkoani Mbeya(Picha na Dailes Razaro)

Katika kuendelea na mfungo wa Ramadhan kwa dini ya Kiislamu tumeshuhudia makundi mbalimbali nchini yamekuwa yakifanya ibada ya kufuturisha maeneo mbalmbali nchini, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera ameandaa chakula cha jioni katika mkoa wake.

Na Dailes Razaro

Wananchi mkoani Mbeya wametakiwa kuendelea kuitunza amani iliyopo kwa kuwa itasaidia kuleta maendeleo kwa wakati sambamba na kuombea taifa

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera wakati wa  akishiriki futari pamoja na waumini wa dini ya kiislamu.

Homera amesema Rais Samia Suluhu Hassan ameleta miradi mingi ya maendeleo hivyo amewasihi viongozi wa dini kuhubiri amani ili miradi hiyo iendelee ndani ya mkoa huo.

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera(Picha na Dailes Razaro)
Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera

Aidha baadhi ya viongozi wa dini wakiwakilishwa na shehe wa mkoa wa Mbeya Issa Bombo ametoa shukrani zao kwa mkuu wa mkoa na serikali kwa ujumla huku akiahidi kuwa wataendelea kuonesha ushirikiano.

Shehe wa mkoa wa Mbeya Issa Bombo(Picha na Dailes Razaro)
Sauti ya shehe wa mkoa wa Mbeya Issa Bombo