Baraka FM

RAS Seneda apongeza ujenzi miradi halmashauri ya wilaya Momba

8 November 2023, 16:06

Katibu Tawala mkoa wa Songwe Bi. Happiness Seneda akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Momba mkoani Songwe (Picha na mwandishi wetu)

Katibu tawala mkoa wa Songwe Bi. Happiness Seneda ameanza rasmi ziara yake ya siku tatu katika halmashauri ya wilaya ya Momba ikiwa ni ufuatiliaji wa miradi ya serikali ambapo pia ameongozana na wajumbe wa timu ya sekretarieti ya mkoa wa Songwe ambapo baada ya kutembelea miradi wamewapongeza sana timu ya halmashauri ya wilaya ya Momba ambayo ipo chini ya mkurugenzi mtendaji Bi. Regina Bieda katika kutekeleza miradi kwa ubora na viwango sahihi.

Katibu tawala mkoa wa songwe bi. Happiness Seneda akikagua josho la kuoshea mifugo halmashauri ya Momba(picha na Mwandishi wetu)

Aidha katibu tawala amewashukuru sana wananchi wa Momba kwa kuwa mstari wa mbele katika kujitokeza kuchangia na kujitoa kwenye miradi mbalimbali ambayo inaletwa na serikali katika vijiji na kata.

“Nawapongeza sana halmashauri ya wilaya ya Momba kwa kweli mnasimamia vyema fedha za miradi zinazoletwa na mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan “

Katibu tawala mkoa wa songwe bi. Happiness Seneda akiendelea na ukaguzi wa miradi halmashauri ya Momba Songwe(Picha mwandishi wetu)
Sauti ya Katibu tawala mkoa wa songwe bi. Happiness Seneda