Baraka FM
Baraka FM
12 December 2024, 15:06

Magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu yamekuwa yakisababishwa na uchafuzi wa mazingira.
Na Hobokela Lwinga
Mganga Mkuu Wa Halmashauri Ya Jiji La Mbeya Yesaya Mwasubila amesema wanaendelea Kuchukua hatua za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Kipindupindu kutokana na watu wanaougua ugonjwa huo kufikia 22.
Hatua hizo ni pamoja na kufunga visima vya Maji Mama Na Baba lishe pamoja na Vilabu vya Pombe ambavyo havikidhi viwango vinavyohitajika.
Hata hivyo licha ya ongezeko la wagonjwa, kakuna kifo kilichoripotiwa na wagonjwa wote wametengewa maeneo maalumu kwa ajili ya matibabu.
Mwasubila amesema idadi ya wagonjwa imeongezeka kutoka 17 walioripotiwa siku nne zilizopita hadi kufikia 22 usiku wa kuamkia jana.