Baraka FM

Wasichana 700 shule ya sekondari Kayuki wapewa taulo za kike

8 October 2023, 07:17

Naibu Waziri wa Maji Maryprisca Mahundi akikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa sekondari Kayuki Rungwe (Picha na mwandishi wetu)

Jukumu la malezi ni la kila mtu, katika kuwezesha mabinti ili kupata elimu kwenye mazingira bora huna budi kuhakikisha mabinti hao wanafunzi wanawekwa kwenye mazingira mzuri kila wakati.

Na mwandishi wetu

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amewapa tabasamu wanafunzi zaidi ya 700 sekondari ya wasichana Kayuki iliyopo wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya kwa kutoa msaada wa taulo za kike zaidi ya 1000 .

Mhe. Maryprisca Mahundi akizungumza wakati wa kukabidhi taulo za kike Kayuki sekondari (picha na mwandishi wetu)

Mhe. Mahundi amewapa fursa za za taulo kwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani kidato cha nne na cha pili wao kila mmoja amepatiwa taulo mbili mbili ilhali kidato cha kwanza,tatu na tano wamepatiwa taulo moja moja.

Mahundi ametumia fursa hiyo pia kueleza dhima ya kuanzisha taasisi yake ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) lengo likiwa ni kusaidia watoto na wanawake kiuchumi kauli mbiu yake Tukue Twende Pamoja.

Picha ya pamoja viongozi wa shule na Maryprisca Mahundi (picha na mwandishi wetu)