Baraka FM

Mgogoro wa ardhi Mbeya wasababisha mapigano, polisi watumia mabomu

11 October 2023, 15:53

Baadhi ya askari wa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya wakiwa eneo la tukio wakiimarisha ulinzi(Picha na Sifael Kyonjola)

Jeshi la polisi limejikuta likitumia nguvu kwa kutumia mabomu ya machozi kuwaondoa wananchi hali iliyoleta taharuki ya mapigano kati ya wananchi na jeshi la polisi.

Na Sifael Kyonjola

Mtaa wa Gombe kata ya Itezi jijini Mbeya umegeuka uwanja wa mapambano ya kivita baina ya wananchi zaidi ya mia moja hamsini wanaotakiwa kuondoshwa kwa amri ya mahakama baada ya wenzao watano kushindwa kesi.

Hili si maigizo bali ni hali halisi iliyotokea kata ya Itezi wananchi wakipambana na polisi kuzuia nyumba zao zisibomolewe na hapa wananchi hao wanapaza sauti zao kuwa mgogoro huo ulikuwa unahusisha watu watano na si wananchi wote.

Baadhi ya wananchi wa kata ya Itezi jijini Mbeya wakiwa wameshika silaha wakati wa makabiliano na jeshi la polisi wakipinga kubomolewa nyumba zao (Picha na Sifael Kyonjola)
Sauti ya baadhi ya wananchi wa Kata ya Itezi wananchi

Diwani wa kata ya ya Itezi Sambwee Shitambala ambaye ni mmoja wa Mawakili wa kujitegemea amesema wahanga wa mgogoro huo ni wananchi zaidi 150.

Diwani kata ya Itezi jijini Mbeya Sambwee Shitambala akizungumza na wananchi eneo la tukio (Picha na Sifael Kyonjola)
Sauti ya Diwani wa Kata ya ya Itezi Sambwee Shitambala

Aidha mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Usalama wilaya Mbeya amekiri kuwepo kwa vurugu eneo la Itezi na amewaomba wananchi kuwa watulivu kipindi hiki ambacho serikali inaendelea kuona amri ya mahakama inatekelezwa.

Mkuu wa wilaya ya Mbeya Beno Malisa akizungumzia mgogoro katika kata ya Itezi akiwa ofisini kwake(picha na Sifael Kyonjola)
Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Beno Malisa

Jiji la Mbeya limekuwa na migogoro mingi ya ardhi inayotokana na mipango mibovu ya mipango miji sanjari na maafisa ardhi kugawa viwanja mara mbili.