Baraka FM

Familia yavamiwa Songwe, mke abakwa

13 March 2024, 09:31

Katika hali isiyo ya kawaida, familia moja mkoani Songwe imejikuta ikiingia kwenye hofu kubwa baada ya kuvamiwa usiku wa manane na kisha mama wa familia kubakwa na watu wasiofahamika.

Na Ezra Mwilwa

Mwanaume mmoja (Jina limehifadhiwa) mkazi  wa wilaya Songwe mkoani Songwe amesema alivamiwa na watu wasiojulikana na kisha kuiba fedha na kisha kumbaka mke wake .

Akizungumza na kituo hiki mtendewa huyo amesema tukio hilo lilitokea  Septemba 5, 2023 majira ya saa sita usiku akiwa nyumbani kwake yeye na familia yake.

Sauti ya mtendwa

Mwenyekiti wa haki za binadamu Mbeya na mkrugenzi wa kituo cha msaada wa kisheria Tarecase Mbeya  Ndg. Said Mohamed amesema kitendo alichofanyiwa kijana huyo ni kitendo cha ukatili na kinyama

Sambamba na hayo Ndugu Said amewashauri wananchi mbalimbali kuendelea kufuatilia elimu zinazotolewa na kitengo hicho kwa ajili ya kujifunza namna ya kuripoti tuhuma mbalimbali wanazokumbana nazo.

Mwenyekiti wahaki za binadamu Mbeya na mkrugenzi wakituo cha msaada wa kisheria tarecase Mbeya  ndg. Said Mohamed (Picha na Ezra Mwilwa)
Sauti ya mwenyekiti wa haki za binadamu Mbeya na mkrugenzi wa kituo cha msaada wa kisheria Tarecase Mbeya  Ndg. Said Mohamed