Baraka FM

Utoro chanzo ufaulu kushuka kwa wanafunzi kidato cha nne

3 October 2023, 17:17

Baadhi ya wahitimu wa shule ya sekondari Shikula iliyopo mkoani Songwe wakiimba wimbo wa kuwaaga wanafunzi wenzao na walimu.(Picha na Rukia Chasania)

Wazazi na walezi ni lazima wawe karibu na watoto wao ili kuhakikisha wanazingatia masomo yao na kufika shuleni kwa wakati ili waweze kufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho.

Na Rukia chasanika

Imeelezwa kuwa utoro wa wanafunzi wa shule ya sekondari Shikula iliyopo kata ya Nanyala mkoani Songwe unasababisha baadhi ya wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katika mitihani yao.

Hayo yamesemwa na diwani wa kata ya Nanyala George Msyani wakati  akizungumza katika mahafali ya 16 ya shule hiyo.

Msyani amesema ili kukomesha tabia hiyo ni lazima wazazi na walimu washirikiane kwa pamoja kukemea tabia hiyo.

Sauti ya diwani kata ya nanyala George Msyani

Pia Msyani ameongeza kuwa ni wajibu wa jamii kuwa na mchango wa kuwasaidia  wanafunzi hao ili kuwaongezea hali ya kuwa na bidii katika masomo .

Mgeni rasmi ambaye ni diwani wa kata ya Nanyala George Msyani akitoa vyeti kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne shule ya sekondari Shikula mkoani Songwe (picha na Rukia Chasanika)

Naye mkuu wa shule hiyo Emmanuel Kayombo amesema shule yao inakabiliwa na changamoto ya upungugu wa walimu wa sayansi na hisabati hivyo wanaiomba serikali iwasaidie.

Sauti ya mwalimu mkuu wa Shikula Emmanuel Kayombo

Akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa niaba ya wanafunzi Ronick Mwankota amesema wamefanikiwa kuendeleza miradi wa ufugaji mbalimbali katika shule hiyo.

Sauti ya mwanafunzi Ronick Mwankota