Baraka FM

Mwaka wa fedha 2023/2024 Rungwe kupanda miti milioni1.5

16 January 2024, 10:25

Na mwandishi wetu

Halmashauri ya wilaya ya Rungwe inatarajia kupanda miche ya miti Millioni 1.5 katika mwaka huu wa fedha 2023/24.

Hii inajumuisha miche iliyopo katika kitalu cha Halmashauri kilichopo Tukuyu mjini na mingine kupitia wadau mbalimbali.

Katika kitalu cha Halmashauri miche hutolewa bure kwa mtu mmoja mmoja na taasisi kwa ujumla.

Miti hii ni ya matunda ,mbao, vivuli na mizuri kuhifadhia vyanzo vya maji.