Baraka FM

DC Mwanziva atembelea gereza la Ludewa, asisitiza uzalishaji mali

13 November 2023, 15:03

Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Mhe. Victoria Mwanziva akiwa na viongozi wa gereza la Ludewa (picha na Josea Sinkala)

Na Josea Sinkala

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Mhe. Victoria Mwanziva, amefanya ziara katika Gereza la Wilaya Ludewa mkoani humo.

Akizungumza na viongozi mbalimbali amesema gereza la Ludewa pamoja na kurekebisha tabia za wafungwa pia lipo ili kuzalisha mazao mbalimbali.

“Gereza hili lipo chini ya Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza (SHIMA), likizalisha wastani wa mavuno wa zaidi ya tani 520 kwa mwaka Gereza hili linatekeleza mradi wa Kilimo likiwa na lengo la kuzalisha chakula cha kutosheleza kuhudumia Gereza hili na Magereza mengine chini ya mradi huu wa SHIMA kwa Mkoa wa Njombe na kitaifa”, amesema Mwanziva.

Pia mkuu huyo wa Wilaya amepongeza mpango uliopo wa wafungwa kupatiwa ujuzi na stadi za kazi zitakazo wasaidia wanaporejea uraini na kusisitiza utaratibu huo uendelee.

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Mhe. Victoria Mwanziva akikagua baadhi ya maeneo ja gereza la Ludewa (picha na Josea Sinkala)

Sanjari na hayo DC Mwanziva, amewashika mkono wafungwa, mahabusu na watumishi wa Gereza la Ludewa kwa kuwapatia mahitaji muhimu mbalimbali.