Baraka FM

Zaidi ya asilimia 34ya Wanafunzi Mbeya walipoti shuleni ndani ya siku tatu

11 January 2024, 18:33

Na mwandishi wetu, Mbeya

Leo Alhamiss Januari 11 2024 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde:Juma Homera ameipokea Kamati ya Kudumu ya Bunge Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Ikiongozwa na M/kit wa Kamati hiyo Denis Lazaro Yondo Mbunge wa Jimbo la Mikumi.

Kamati hiyo ikapata Nafasi ya kusikiliza Taarifa Kutoka Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini(TARURA) kadharika Hali ya Elimu kwa Mkoa Wa Mbeya iliyowasilishwa na Meneja Wa TARURA Mkoa kadharika Elimu Zaidi ya Wanafunzi Elfu 16 ambao ni zaidi ya Asilimia 34 ya tayari Wamesharipoti Shuleni Mwaka huu 2024 ikiwa ni Siku Tatu zimepita tangu Shule kufunguliwa.

Wajumbe wa Kamati hiyo akiwemo Mbunge wa Tarime Mh: Mwita Waitara wamempongeza RC Homera na Kumuomba aongeze Kasi ya kufatilia na kuhamasisha Wanafunzi kuripoti Shuleni.

Naibu Waziri Wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Deogratus John Ndijembi akaihakikishia Kamati kuwa Swala la Wanafunzi kuripoti Mashuleni Litakwenda Vizuri kama Wizara Watahakikisha Maagizo ya Waziri yanatekelezwa ikiwemo ya Sare na Dhana zingine Kutokuwa kikwazo Cha kumzuia Mwanafunzi kuripoti Shule.

Mwisho M/kit wa Kamati akahitimisha Kwa Kuishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kuendeleza Jitihada za Mh:Rais za kuwapigania Wananchi katika kusimamia Miradi mbali mbali ya Maendeleo hasa kwa Mkoa wa Mbeya.