Baraka FM

Epukeni watumishi matapeli, wanawapapasa mnatoa hela

31 December 2023, 14:06

Makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch.Asulumenye Mwahalende (Picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga

Makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi Mch. Asulumenye Mwahalende ameyataka makanisa yote ya Kanisa la Moravian jimbo la Kusini Magharibi kuhakikisha yanakuwa na kengele ambazo zitakuwa zikipigwa kabla ya ibada ikiwa ni kuwakumbusha waumini na wasio waumini muda wa ibada.

Maagizo hayo ameyatoa wakati akitoa salamu za jimbo akiwa katika ibada maalum ya kumsimika mchungaji wa ushirika Mch. Paul Mwampamba katika ushirika wa Yeriko.

Mchungaji Paul Mwampamba akisimikwa kuwa Mchungaji wa ushirika wa Yeriko kanisa la Moravian (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulumenye Mwahalende

Mchungaji Mwahalende amesema ni utaratibu wa kanisa kuhakikisha utaratibu huo unafuatwa iwe kwa makanisa yaliyojengwa au yanayotarajiwa kujengwa.

Katika hatua nyingine amewataka waumini kuwa makini na watumishi kwani siku za hivi karibu wamejitokeza matapeli wanaotapeli watu kwa kutumia neno la Mungu.

Baadhi ya waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Yeriko Mbalizi (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulumenye Mwahalende

katika kuendelea kuuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024 hapa ushirikani Yeriko Moravian kumeandaliwa semina ya neno la Mungu ambayo ilianza Dec17,2023 na itahitimishwa January 28,2024.