Baraka FM

Baada ya ushindi wa urais wa IPU Dkt. Tulia aandaliwa mapokezi maalum Mbeya

5 November 2023, 13:31

mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela(Kulia)akiwa na Katibu Siasa na  Uenezi Mkoa wa Mbeya ndugu Christopher Uhagile (picha na Hobokela Lwinga)

Baada ya kushinda urais wa IPU Dkt Tulia Akson Mwansasu alifanyiwa mapokezi maalum jijini Dodoma kabla ya kuanza kwa shughuli za bunge ambapo viongozi mbalimbali walijitokeza kumpokea,wakati vikao vya bunge vikiwa vinaendelea jijini dodoma tayari jimboni kwakwe maandalizi ya kumpokea yameanza kwa kushirikiana na halmashauri zote mkoani Mbeya.

Na Hobokela Lwinga

Baada ya mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Akson Mwansasu kushinda urais wa umoja wa mabunge duniani (IPU)Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya kimetoa maagizo kwa kila Halmashauri kushiriki mapokezi ya kumpokea pindi atakapo maliza shughuli zabunge jijini dodoma.

Maagizo hayo yametolewa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela wakati akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi mdogo wa CCM uliopoeneo la sokomatola jijini mbeya.

katika hatua nyingine mnec huyo amewahakikishia wananchi wa mkoa wa mbeya kwamba chama kupitia serikali itaendelea kutatua kero zote zinazowakabiri.

Sauti ya mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela

Katika hatua nyingine Chama hicho kimemtambulisha Katibu Siasa na  Uenezi Mkoa wa Mbeya ndugu Christopher Uhagile

akitoa shukrani baada ya uteuzi huo ndugu Uhagile amemushukru mwenyekiti wa chama hicho Dkt Samia Suluhu Hassan na chama kwa ujumla kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kukitumikia kwa wadhifa huo katika mkoa wa mbeya na amewaviarika vyama vingine vya siasa kutoa maoni na ushauri ili kuujenga mkoa wa mbeya kwenye maendeleo.

Katibu Siasa na  Uenezi Mkoa wa Mbeya ndugu Christopher Uhagile (kushoto)akiwa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela
Sauti ya Katibu Siasa na  Uenezi Mkoa wa Mbeya ndugu Christopher Uhagile