Baraka FM

Chunya yafanikiwa kujenga na kukamilisha miradi ya maendeleo

1 February 2024, 17:36

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Tamim Kambona(Picha na Hobokela Lwinga)

Na Hobokela Lwinga

Wilaya ya Chunya mkoani mbeya imesema kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 2021-2023 imefanikiwa kujenga jengo la utawala lenye thamani ya Zaidi ya  billion mbili.

Akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkutano na waandishi wa habari kati ya mkuu wa mkoa na msemaji mkuu wa serikali,mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Tamim kambona amesema tayari jengo limeanza kutumika.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chunya Tamim Kambona

Aidha katika sekta ya afya Kambona amesema wametumia zaidi ya shilingi bilioni 6 kukamilisha miradi ya afya ikiwemo mradi wa hospitali ya wilaya ya chunya,vituo vya afya vitano sambamba na miradi ya elimu katika halmashauri hiyo.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chunya Tamim Kambona

Mkurugunzi huyo ameendelea kwa kusema kuwa wilaya yake inategemea zaidi madini katika ukusanyaji wa mepato hivyo wameendelea kuboresha na kuweka mazingira mazuri kwa wachimbaji hali ambayo imeongeza ongezeko la wachimbaji.

Sauti ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya chunya Tamim Kambona

Awali akizungumza kwenye mkutano huo mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amesema zaidi ya shilingi bilioni 5 zimetolewa kukamilisha miradi ya afya katika mkoa wake.

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera

Kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Halmashauri ya wilaya ya chunya ina Zaidi ya watu 233,000 huku Zaidi ikitegemewa katika uchimbaji wa dhahabu na zao la Tumbaku