Baraka FM

Lulandala:Iweni walinzi na watetezi wa chama na serikali

10 November 2023, 16:17

katibu mkuu wa UVCCM Fakii Lulandala(Picha na Hobokela Lwinga)

katibu mkuu wa UVCCM Fakii Lulandala amewataka vijana wa UVCCM kuwa walinzi na watetezi wa chama na serikali katika utekelezaji wa maendelo kupitia ilani ya CCM.

Wito huo ameeutoa katika ofisi za chama cha mapinduzi sokomatola jijini mbeya wakati akizungumza na vijana wa chama hicho namna ambavyo wanapaswa kuwajibika katika kukijenga chama.

Aidha katika ziara mkoani mbeya katibu mkuu anatarajia kuhudhuria mapokezi ya rais wa umoja wa mabunge duniani IPU yanayotarajia kufanyika katika viwanja vya ruanda nzovwe jijini Mbeya jumamosi November 11,2023.

katibu mkuu wa UVCCM Fakii Lulandala Akizungmza na vijana katika ofisi cha CCM mkoa wa Mbeya(Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya katibu mkuu wa UVCCM Fakii Lulandala

Sambamba na hayo  Mjumbe wa mkutano mkuu taifa mkoa wa Mbeya ndg.Ndele Mwaselela amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kumpokea spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa Jimbo la mbeya dkt Tulia akson mwansasu katika mapokezi ya kumpongeza kwa kushinda kiti cha urais wa mabunge dunia IPU.

 Mjumbe wa mkutano mkuu taifa mkoa wa Mbeya ndg.Ndele Mwaselela(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya  Mjumbe wa mkutano mkuu taifa mkoa wa Mbeya ndg.Ndele Mwaselela

kwa upande wake katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbeya mjini philimoni mng’ong’o ameshukru Rais dkt samia kwa kumruhusu dkt tulia kugombea nafasi hiyo.

Sauti ya katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbeya mjini philimoni mng’ong’o