Baraka FM

Wananchi watakiwa kutumia michezo kuimarisha afya zao

27 April 2024, 00:11

Mkurugenzi wa shirika la DSW linalojishughulisha na afya na maendeleo kwa vijana(picha na Rukia Chasanika)

Afya ni mtaji jambo lolote ili uweze kulifanya linategemea afya njema hata hivyo wataalamu wa afya wanasisitiza kutunza afya kwa njia ya mazoezi kwani mazoezi yanatajwa kuwa tiba ya kuuokoa mwili wako usipatwe na magonjwa.

Na Rukia Chasanika

Ikiwa leo ni maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Mbeya wameadhimisha kwa siku hii kwa kushiriki katika bonanza la afya katika michzo mbalimbali Ili kuimarisha afya zao.

Akizungumza na wanavyuo hao mkurugenzi wa shirika la DSW linalojishughulisha na afya na maendeleo kwa vijana ambao ndio wadhamini wa michezo hiyo peter Luwaga amesema michezo inawaleta vijana pamoja.

Luwaga amesema wamewapongeza vijana waliaanda bonaza hilo la michezo kwani michzo ni afya.

Katika bonanza hilo shirika la DSW wametoa zawadi mbalimbali kwa washindi ikiwepo mipira ,medani, ngao, mbuzi na kuku.