Baraka FM

Dc Batenga amtaka mkurugenzi kuhakikisha klabu zote mashuleni zinakuwa na walimu walezi

27 February 2024, 19:34

Na Mwandishi wetu

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mhe. Mubarak Alhaji Batenga amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Chunya ndugu Tamim Kambona kuhakikisha Klabu zote zilizopo Mashuleni zinakuwa na walimu walezi pamoja na kuhakikisha wanajengewa uwezo ili waweze kuzisimamia vyema klabu hizo ili klabu zitekeleze lengo lake ipasavyo.

Maagizo hayo ameyataka Wakati wa Maadhimisho ya siku ya mwazilishi wa Skauti duniani ambapo Halmashauri ya wilaya ya Chunya yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kipoka kata ya Bwawani na Mkuu wa wilaya ya Chunya alikuwa Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo

“Natoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji kuhakikisha kwamba haya maeneo yote yani klabu ya Skauti , klabu ya kupinga rushwa, klabu ya mali hai ,klabu ya lishe na Ukimwi klabu zote hizi zipate walimu walezi na ziwe na wanachama kuanzia Shule za Msingi hadi Sekondari kwasababu huko ndiko tunakoaanza kuwaandaa na kuwajenga hawa vijana kuwa wazalendo kwaa Taifa lao “alisema Mhe.Batenga

Aidha Batenga aliongeza kuwa ni vizuri wanafunzi kujitafutia sifa za ziada wanapokuwa shule kwa kujiunga na klabu mbalimbali ambazo zitawawezesha kujifunza mambo mengi yenye manufaa kwao na taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na kuwajenga kuwa wazalendo na taifa lao ,watunzaji wa mazingira , wapinga rushwa pamoja na mambo mengine lakini pia klabu zitawasaidia katika maisha yao ya baadae kwenye soko la ajira.

“Sifa za ziada na misingi ya uzalendo itajengwa kupitia Skauti , kilabu za kupinga rusha , Lishe ,Ukimwi na klabu za mali hai tunasema hawa ni wazalendo kupitia matendo kwani uzalendo ni vitendo tukakupima uzalendo