Baraka FM

Polisi Mbeya kuwasaka watuhumiwa mauaji ya mwalimu, mwanafunzi Chunya

2 April 2024, 07:30

Mwalimu aliyeuawa Chunya mkoani Mbeya

Mwili wa mwalimu aliyeuawa wilaya ya Chunya mkoani Mbeya utasafirishwa kwenda kufanyiwa mazishi mkoa wa Iringa.

Na Ezekiel Kamanga

Mwili wa aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi Mbugani Herieth Lupembe (37) aliyeuawa na watu wasiojulikana utasafirishwa kwenda mkoani lringa kwa ajili ya maziko huku mwili wa lvon Tatizo Haonga (15) mwanafunzi kidato cha kwanza sekondari ya lsenyela kata ya Mbugani utazikwa kata ya Mbugani.

Akitoa taarifa Mwenyekiti wa kijiji cha Mbugani Gideon Kinyamagoha amesema baada ya taratibu za uchunguzi kukamilika miili itakabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Baadhi ya wananchi wakiwa wamejawa na manjozi kutokana na tukio la mauaji (picha na Ezekiel Kamanga)

Baba mzazi wa mwanafunzi aliyeuawa Fackson Simchimba amesema baada ya mazishi watapeleka msiba kwao Mbozi mkoani Songwe.

Sauti ya Baba mzazi wa mwanafunzi aliyeuawa Fackson Simchimba

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba wanaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha mauaji na wahusika.

Sauti ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Benjamin Kuzaga