Baraka FM

Abiria fichueni wanaoshabikia mwendokasi

21 December 2023, 08:23

Na Moses Mbwambo,Iringa

Mkuu wa Usalama barabarani Mkoa wa Iringa (SSP) Mossi Ndozero amewataka abiria kuacha tabia ya kushabikia mwendokasi na badala yake kufichua wote watakaobainika kuendeleza vitendo hivyo.

Ndozero Ametoa kauli hiyo huko Nyigo Wilayani Mufindi, mpakani mwa Iringa na Njombe alipokua akitoa elimu kwa madereva na abiria ikiwa ni operesheni ya usalama barabarani inayohusisha Mikoa hiyo miwili (INTER REGIONAL OPERATION). 

Aidha, aliwataka madereva Kuepuka vitendo vya ulevi na matumizi ya madawa ili kuepuka madhara ya afya ya Akili na Mwili, lakini pia abiria Wamekumbushwa Kampeni ya mpango wa Safiri salama na Abiria Paza Sauti (APS) kwa kukemea matendo hatarishi ya madereva na kutoa taarifa kupitia namba za simu za viongozi.