Baraka FM

Wavenza: Saidieni watoto yatima waishi kama watoto wengine

17 October 2023, 17:30

Hiki ni moja ya kibao kinachotambulisha uwepo kituo cha kulea watoto yatima eneo la Mbozi misheni mkoani Songwe.

Kwenye jamii kuna msemo unasema motto wa mwenzako ni wako ,hii inamaana kuwa kila mtoto anapaswa kupata mahitaji  yote kama watoto wengine unapopata nafasi ikiwa ni pamoja na chakula,elimu na malazi.

Na Deus Mellah

Jamii nchini imetakiwa kuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia watoto wenye uhitaji wanaoishi katika mazingira magumu ili nao waweze kujikimu kimaisha.

Wito huo umetolewa na msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Mbozi mission Annis Wavenza baada ya watoto wa shule ya Jumapili  kutoka kanisa la Moraviani ushirika wa Saza Chunya kutembelea kituo hicho kilichopo eneo la mbozi mission mkoani wa Songwe.

Msimamizi huyo Wavenza amesema kituo hicho kwa sasa kina watoto tisa na wengine wapo shule mbalimbali wanasoma.

Msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Mbozi mission    Annis Wavenza(picha na Deus Mellah)
Sauti ya Msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Mbozi mission    Annis Wavenza

Naye mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi ushirika wa Saza  Chunya  Enerd Mwashibale amewashukuru wasimamizi wa kituo hicho kwani wamekuwa wakiwahudumia    watoto  mbalimbali bila kujali dini wala kabila.

Mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi     ushirika wa Saza  Chunya  Enerd Mwashibale(picha na Deus Mellah).
Sauti ya mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi     ushirika wa Saza  Chunya  Enerd Mwashibale

Nao baadhi ya watoto wa shule ya jumapili pamoja na walimu wao wamesema wamewasaidia watoto hao mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni,Nishati umeme(solar) pamoja na nguo.

mchungaji wa kanisa la Moravian Tanzania jimbo la kusini Magharibi     ushirika wa Saza  Chunya  Enerd Mwashibaleakiwa na watoto wa shule ya jumapili ushirika wa Saza Songwe
Sauti za baadhi ya watoto wa shule ya jumapili pamoja na walimu wao