Baraka FM

PM Majaliwa kufungua kongamano la idhaa ya kiswahili jijini Mbeya

18 March 2024, 12:08

Waziri mkuu kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi mbalimbali waliofika kumpokea katika uwanja wa ndege wa Songwe Mbeya (picha na Hobokela Lwinga).

Kiswahili ni moja ya lugha ya mawasiliano ambayo inaendelea kukua kwa kasi ambapo kwa sasa mataifa mbalimbali duniani yamekuwa yakiitumia kuwasiliana.

Na Hobokela Lwinga

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kasim Majaliwa Majaliwa amewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe uliopo mkoani Mbeya na kupokelewa na mwenyeji wake Juma Homera ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.

Mh. Majaliwa amewasili mkoani huo kwaajili ya kufungua Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani linalofanyika kuanzia leo March 18 – 22, 2024 katika Ukumbi wa Eden Highlands Hotel, Jijini Mbeya.