Baraka FM

UVCCM Mbeya yaipongeza serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan

26 October 2023, 14:17

Mwenyekiti wa umoja huo Yassin Ngonyani akizungumza na viongozi wa UVCCM kutoka ngazi ya wilaya(picha na Ezra Mwilwa)

Unapofanya jambo zuri na lenye tija kwa jamii ni lazima upongezwe,hivyo ukiwa binadamu mwenye utu unapopewa nafasi ya kuongoza watu wa jamii yako huna budii kuacha alama nzuri ili kesho yako uweze kupongezwa.

Na Ezra Mwilwa

Umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM mkoa wa Mbeya wameipongeza Serikali inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa  kuendelea kufanya ukarabati wa miundombinu.

Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa umoja huo Yassin Ngonyani katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa umoja huo kujadili mipango ya ndani ya umoja na chama kwa ujumla.

Sauti ya mwenyekiti wa umoja huo Yassin Ngonyani

Ngonyani amesema wanaipongeza serikari kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara nne ndani ya jiji la Mbeya na kukarabati wa miundombinu katika sekta ya elimu na kilimo.

Mwenyekiti wa umoja huo Yassin Ngonyani (picha na Ezra Mwilwa)

Pia amesema watahakikisha wanafikia makundi maalumu ili kupata changamoto wanazopitia na kuhakikisha wanazifikisha katika mamlaka husika ili zitatuliwe kwa wakati.

Sauti ya mwenyekiti wa umoja huo Yassin Ngonyani