Baraka FM

Ndoa 16 zafungwa na kubarikiwa siku moja ya mwaka mpya

1 January 2024, 13:08

Na Hobokela Lwinga

katika kuupokea mwaka mpya 2024 kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Yeriko uliopo mbalizi Mbeya.

Akiongoza katika ibada hiyo kwa wanandoa hao mchungaji wa ushirika wa Yeriko Paul Mwampamba amesema ndoa hizo ni mwanzo katika kuupokea mwaka hivyo wanatarajia miezi ijayo ikiwemo pasaka kufungwa nyingi zaidi.

Mchungaji wa ushirika wa Yeriko Paul Mwampamba(Picha na Hobokela Lwinga)

Hata hivyo mchungaji huyo amewataka waumini ambao bado hawafunga ndoa na kubariki kujitathimini na kisha kuchukua hatua ya kufanya hivyo.

Akihubiri katika ibada hiyo maalumu ya wanandoa hao mtume Asifati Mwasenga amesema wanandoa wanatakiwa kutunziana siri na kupeana heshima ili ndoa zao ziendelee kuwa salama.

Mtume Asifati Mwasenga (Picha na Hobokela Lwinga)