Baraka FM

Waumini watakiwa kuachana na tabia za unafiki ndani ya dini zao

23 October 2023, 13:25

Baadhi ya waumini na waimbaji katika mkutano wa jimbo kutoka wilaya zote za kanisa la Moravian jimbo la Kusini Magharibi (Picha na Hobokela Lwinga)

Mtu anapoamini ni ishara ya kufanya vitu vingi kwenye maisha ndivyo ilivyo pia mtu akiamini katika imani ya dini anapaswa kuishi maisha kulingana na imani ya dini yake, kwa wakristo wanaaswa kuishi maisha kama aliyoishi Yesu akiwa duniani.

Na Hobokela Lwinga

Kanisa la Moravian Tanzania jimbo la Kusini Magharibi limefanikiwa kufanya mkutano mkuu wa kwaya kuu katika ushirika wa Mlima Reli huku mkutano mwingine kama huo ukitarajiwa kufanyika mwakani 2024 katika kanisa la Moravian eneo la  Misheni ya Iringa.

Katika hali hiyo makamu mwenyekiti na mlezi wa idara ya kwaya kuu jimbo la Kusini Magharibi  Mch. Asulumenye Mwahalende amemuelekeza mwenyekiti wa misheni ya Iringa Mch. Bora Msola kuandaa mazingira mazuri  ya kupokea ugeni huo ambao utakuwa na washiriki zaidi ya 400.

Mch. Mwahalende amewatakia viongozi wote kuanzia ngazi ya ushirika  maandalizi mema ya mikutano kwa mwaka ujao .

Makamu mwenyekiti na mlezi wa idara ya kwaya kuu jimbo la kusini magharibi  mch.Asulumenye Mwahalende (picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya makamu mwenyekiti na mlezi wa idara ya kwaya kuu jimbo la Kusini Magharibi  Mch. Asulumenye Mwahalende.

Wakati akihubiri katika ibada hiyo mwenyekiti wa misheni ya iringa kaninsa la Moravian Mch. Bora Msola amewataka waumini kuacha tabia ya unafiki katika kufanya kazi ya Mungu.

Mwenyekiti wa misheni ya iringa kaninsa la Moravian Mch. Bora Msola (Picha na Hobokela Lwinga)

Sambamba na hayo mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania wilaya ya mbalizi mch.Erica Samwanijembe amelishukru jimbo kwa kufanya mkutano huo wilayani kwake.

Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania wilaya ya mbalizi mch.Erica Samwanijembe(picha na Hobokela Lwinga)
Mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania wilaya ya mbalizi mch.Erica Samwanijembe

Hata hivyo katibu wa idara ya kwaya na uinjilisti jimbo la kusini magharibi mch.Peter mbugi  Amewashukru washiriki wote wa mkutano kwa namna ambavyo wamejitoa katika kumtumikia mungu.

Kwa upande wake mshindi wa mziki katika mkutano huo Kisa Kayuni amelishukru kanisa kwa kutambua vipaji,na vipawa kwa waumini wake.

Mshindi wa mziki katika mkutano huo Kisa Kayuni akipokea chti cha kutambua ufaulu wa somo la muziki(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya mshindi wa muziki katika mkutano huo Kisa Kayuni