Baraka FM

Mch. Mwampamba asimikwa kuwa mchungaji ushirika wa Yeriko, katibu Mbalizi

31 December 2023, 15:02

Na Hobokela Lwinga

Mchungaji Paul Mwampamba hatimaye amesimikwa rasmi kuwa Mchungaji wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi ushirika wa Yeriko na katibu wa wilaya ya Mbalizi inayopatikana katika mji mdogo wa Mbalizi halmashauri ya wilaya ya Mbeya.

Ibada ya kusimikwa kwa mchungaji huyo imeongozwa na Makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulumenye Mwahalende amemtaka Mchungaji huyo kuongoza ushirika huo kwa neema ya Mungu kwa ushirikiano na watumishi wengine atakao saidiana nao.

Makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulumenye Mwahalende(picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Makamu mwenyekiti wa kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi mch.Asulumenye

Akizungumza baada kusimikwa mchungaji Paul Mwampamba ameomba ushirikiano kwa waumini huku akiomba kila mmoja kumuombea na kuliombea kanisa.

Mchungaji wa ushirika wa kanisa la Moravian Tanzania ushirika wa Yeriko mch.Paul Mwampamba akiwa na mke wake Scola Ndongole(Picha na Hobokela Lwinga)
Sauti ya Mchungaji wa ushirika wa kanisa la Moravian Tanzania ushirika wa Yeriko mch.Paul Mwampamba

Akizungumza kwa niaba ya baraza na waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Yeriko Meshack Mlawa amesema ni mpango wa Mungu mchungaji Mwampamba kuletwa ushirikani hapo katika kuendeleza mipango uliyopo ushirikani hapo.

Sauti ya mwakilishi wa baraza na waumini wa kanisa la Moravian ushirika wa Yeriko Meshack Mlawa