Baraka FM

Magonjwa zaidi ya 290 yanasababisha afya ya akili

11 October 2023, 12:58

Mtangazaji Kelvin Lameck (kulia)akiwa na msaikolojia Daniel Ndagamusu (kushoto)wakizungumza ndani ya studio za baraka fm(picha na Rachel Malango)

Katika kukabiliana na ugonjwa wa afya ya akili wananchi wanashauriwa kufika kwenye vituo vya afya vinavyotoa huduma za afya ili kupima na kujua hali zao.

Na Rachel Malango

Tanzania inaungana na mataifa mengine ulimwenguni kuadhimisha kilele cha siku ya afya ya akili ambayo hufanyika kila ifikapo Oktoba 10 kila mwaka ambapo kwa hapa nchini inaadhimishwa mkoani Dodoma.

Akizungumzia Maadhimisho hayo Mwanasaikolojia kutoka hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya Daniel Ndagamusu amesema kuwa tatizo la afya ya akili linasababishwa na magojwa Zaidi ya 290.

Ndagamusu amesema kuwa tatizo la afya ya akili linaweza kusababishwa na ukatili mtu anaofanyiwa akiwa mtoto, changamoto za kimaisha, ajali na magonjwa ya kurithi.

Mwanasaikolojia kutoka hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya Daniel Ndagamusu(picha na Rachel Malango)
Sauti ya Mwanasaikolojia kutoka hospitali ya rufaa ya kanda ya Mbeya Daniel Ndagamusu

Mmoja wa Wananchi jijini Mbeya Fadhili Ally amesema kuwa ugonjwa wa afya ya akili unatokana na changamoto za ulevi na ugumu wa maisha hivyo wanawaomba wataalamu kuendelea kutoa elimu.

Mwandishi wa Baraka fm Rachel Malango akifanya mahojiano na mwananchi jijini Mbeya Fadhili Ally
Sauti ya mwananchi jijini Mbeya Fadhili Ally