Baraka FM

Afisa tarafa akerwa na watendaji wazembe

20 March 2024, 16:47

Afisa Tarafa ya Ilongo Magdalena Sikwese(picha na mwandishi wetu)

Unapoaminiwa na kupewa kufanya kazi fulani huna budi kuonyesha jitihada zako za utendaji kazi kwa weledi.

Na mwandishi wetu

Afisa Tarafa ya Ilongo Magdalena Sikwese ameagiza Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanatumia nafasi zao kwa kuwatumikia Wananchi vizuri ikiwemo kuwa na kauli nzuri, kuwa wakarimu, kusoma mapato kwa wananchi, kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.

“Watendaji tumeshau wajibu wetu wa kusoma mapato na matumizi. Sisi Watendaji tumefika kwenye maeneo ya Wananchi tukajifanya nasisi wananchi, tumesahau kwamba hao Wananchi tumewafahamu baada ya kupata ajira hapo.”

Magdalena Edwin amesema unaposoma taarifa za mapato na matumizi kwa Wananchi inatia moyo hata utakapowaomba michango mingine ya kimaendeleo itakuwa rahisi kujitoa