Baraka FM

Makanisa ya askofu Gwajima yafungwa Mbeya

6 June 2025, 21:53

kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga

Wakati waumini wa kanisa la ufufuo na uzima wakiwa katika sintofahamu kubwa juu ya wapi pa kuabudu, serikali imeendelea kuyafungia makanisa hayo nchi nzima.‎‎

Na Hobokela Lwinga ‎‎‎

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeyafunga makanisa sita ya Ufufuo na Uzima yaliyopo eneo la ZZK Mbalizi, Mtaa wa Mnadani Rujewa Wilaya ya Mbarali, Wilaya ya Chunya, Rungwe, Kyela na Jijini Mbeya.

‎‎Taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga amesema wameyafungia makanisa hayo Kufuatia tamko la serikali lililotolewa Juni 02, 2025 kupitia msajili wa jumuiya za kiraia nchini la kufunga makanisa ya Ufufuo na Uzima kutoendelea kutoa huduma katika matawi yake yote yaliyopo nchi nzima.‎‎

Kamanda Kuzaga amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kufanya ufuatiliaji ili kubaini uwepo wa makanisa hayo na kuchukua hatua za kisheria.