Baraka FM

Fahamu faida, hasara za mionzi kwenye mwili wa binadamu-Kipindi

11 April 2024, 13:32

Katikati kutoka kulia ni Peter Ngamilo mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atom Tanzania TAEC, kushoto ni Fred Monyo Afisa Ukaguzi Usalama wa Mionzi (TAEC) Picha na Hobokela Lwinga

Na Hobokela Lwinga

Kutokana na uelewa mdogo wa mionzi kwa wananchi, jamii imetakiwa kuipokea elimu ya mionzi pindi wataalum wanapofika kwenye maeneo yao kwani kufanya hivyo kutaepusha magonjwa yatokanayo na athari za mionzi ikiwemo saratani.