Baraka FM

Kambi ya madaktari bigwaa Mbeya yaleta furaha kwa wananchi

16 April 2024, 15:34

Dkt. Boniface Kavevele Daktari Bigwaa wa upasuaji wa Mishipa ya fahamu, ubongo na uti wa mgongo( Hospital ya Rufaa ya kanda Mbeya)

Wananchi mkoani Mbeya wamepata huduma za matibabu bure kupitia Hospitali ya Kanda ya Rufaa Mbeya.

Na Ezra Mwilwa

Kutokana na ushirikiano wa wataalamu wa Afya kutoka Hospital ya Taifa Mhimbiri kuweka kambi Mbeya matunda ya kambihiyo, wananchi 280 wamenufaika

Dkt. Boniface Kavevele ameeleza mafanikio waliyo yapata baada ya kutamatika kwa kambi ya Madaktari Bigwa kutoka Hospital ya Taifa Mhimbiri kuweka kambi Mbeya juu ya upasuaji wa mishipa ya Fahamu, Ubongo na Uti wa mgongo.

Dkt. Kavevele amesema wananchi zaidi ya 280 watapatiwa huduma za matibabu kati yao wagonjwa 36 wanafanikiwa kufanyiwa upasuaji na kuahidi kuwa wao kama Madaktari Bigwa wataende kutoa huduma hiyo baada ya kambi hiyo kutamatika.

Sauti ya Dkt. Boniface Kavevele