Baraka FM

Serikali kuboresha miundombinu ya huduma za afya

2 December 2023, 08:33

Na Kelvin Lameck

Serikali imesema itaendelea kuboresha miundombinu ya utoaji wa huduma za afya sambamaba na kutoa elimu kwa Wananchi ikiwa ni hatua ya kukabiliana na kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi.

Hayo yamesemwa na mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila wakati akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambayo kwa wilaya hiyo yamefanyika viwanja vya shule ya sekondari Chimala.

Mwila amesema kasi ya maambukizi kwa wilaya ya Mbarali ni asilimia 9.3 wakati kwa chimala pekee ni asilimia 14.3 na Wagonjwa waliojisajili ni 3,545 hivyo Wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila(picha na Kelvin Lameck)
Sauti ya mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Mwila

Akisoma risala Mbele ya mgeni rasmi Evance Ngalawa amesema halmashauri itaendelea kuziimarisha kamati zinazohusika na kupambana na ukimwi ili ziweze kufuatilia mipango na taarifa zitakaowezesha kuzuia maambukizi mapya.

Baadhi ya wanafunzi wakitumbuiza katika maadhimisho (picha na Kelvin Lameck)
Sauti ya msoma risala Mbele ya mgeni rasmi Evance Ngalawa

Nae Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Mbarali Groly Komba amesema kila mtu ana wajibu wa kushiriki katika kupambana na maambukizi ya Virusi vya ukimwi kuanzia kwenye ngazi ya familia.

Sauti ya Afisa Maendeleo wa Wilaya ya Mbarali Groly Komba

Hata hivyo mmoja wa waathirika wa ugonjwa huo ameishukuru serikali kwa kutoa bure dawa za kufubaza makali ya ugonjwa wa ukimwi huku akiwataka watu wengine kupima afya zao.

Sauti ya mmoja wa waathirika wa ugonjwa wa ukimwi

Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani hufanyika kila mwaka ifikapo disemba mosi ambapo kwa mwaka huu yameambatana na kaulimbiu isemayo “JAMII IONGOZE KUTOKOMEZA UKIMWI”.