Baraka FM

Wazazi washauriwa kutengeneza mazingira mazuri kuondoa utoro kwa wanafunzi

17 October 2023, 15:48

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne shule ya sekondari Imezu Mbeya(picha na Deusi Mellah)

Mazingira mazuri kwa wanafunzi kunatajwa kuwa chanzo cha mafaniko kwa wananfunzi wengi, wanafunzi wengi wameshindwa kufanya vizuri kwenye masomo yao kwa sababu ya kukutana na changamoto kwenye mazingira ya shule na nyumbani.

Na Deus Mellah

Wazazi na walimu kwa kushirikiana kwa pamoja  wanaweza kutatua  tatizo la utoro wa wanafunzi   katika shule  ya sekondari Imezu iliyopo kata ya Inyala mkoani Mbeya.

Hayo yamesemwa na mwalimu mkuu wa shule hiyo Ferdinand Skuliet  wakati akizungumza na kituo hiki kuhusu namna walivyoshirikiana na wazazi kutokomeza utoro katika shule hiyo.

Amewataka wanafunzi wanaojiandaa na mtihan wa taifa kuwa watulivu wakati wakisubiri mtihani huo.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Ferdinand Skuliet  akizungumza na wanafunzi wahitimu (Picha na Deusi Mellah)
Sauti ya mwalimu mkuu wa shule hiyo Ferdinand Skuliet

Naye Elizabet Mbwete ambaye ni mwenyekiti wa bodi katika shule hiyo amewaasa wanafunzi hao kuendelea kujisomea ili kila mmoja aweze kufaulu.

Pichani ni Elizabet Mbwete mwenyekiti wa bodi akizungumza na wanafunzi wahitimu (picha na Deusi Mellah)
Sauti ya Elizabet Mbwete mwenyekiti wa bodi

Mmoja wa wanafunzi wanaoenda kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne amesema amejianda vizuri katika mtihani utakaoanza  nov 13,mwaka huu.

Sauti ya wanafunzi sekondari Imezu